MKULAZI IMESAINI MKATABA WA MAUZIANO YA SUKARI NA BODI YA NAFAKA MCHANGANYIKO
Mtendaji Mkuu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi(MHCL) Selestine Some (kushoto) akimkabidhi Mkataba wa mauziano ya sukari Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Patrick Magologozi Mongella(kulia). Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya Kampuni Hodhi ya Mkulazi na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko yaliyofanyika leo kwenye Ofisi za MHCL mkoani Morogoro Septemba 24, 2024.