Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi Mitambo wa Kitengo cha Boiler

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na matengenezo ya kinga (preventive maintenance) ya mifumo na vifaa vya mitambo;
  2. Kufanya kazi za kufunga, kuunganisha, kusakinisha na kupanga kwa usahihi (alignment) sehemu za mitambo na mashine za mfumo wa boiler pamoja na vifaa vyake saidizi, ikiwemo pampu, feni, conveyor, gearbox, turbine, vali na mifumo ya mabomba;
  3. Kufanya ukarabati, kubadilisha na kurekebisha sehemu za mitambo zenye hitilafu kama vile bearing, gear, shaft, pampu na coupling;
  4. Kutumia kwa usalama na ufanisi zana nzito za mkono na zana zinazoendeshwa kwa umeme katika kazi za matengenezo ya mitambo;
  5. Kutengeneza miundo rahisi ya vyuma na vipuri mbalimbali kwa ajili ya shughuli za ukarabati na matengenezo;
  6. Kushiriki katika ukarabati mkubwa wa vifaa (overhauls), matengenezo wakati wa kusimamisha uzalishaji (shutdown maintenance) na ukarabati mkubwa wa mashine;
  7. Kusaidia katika usakinishaji na majaribio ya vifaa vipya vya mitambo;
  8. Kuhakikisha usafi wa eneo la kazi na mazingira salama wakati wa kutekeleza shughuli za matengenezo ya mitambo;
  9. Kuripoti kwa msimamizi hatari zinazoweza kutokea, kasoro za mashine na hali zisizo za kawaida zinazoonekana wakati wa uendeshaji au matengenezo ya nje ya msimu wa uzalishaji (off-crop maintenance);
  10. Kutunza kumbukumbu na kuandaa taarifa za kazi zilizofanyika, vipuri vilivyotumika na zana zilizotumika katika shughuli za ukarabati, huduma, overhaul, fitting na usakinishaji wa mashine;
  11. Kutunza kumbukumbu na kuandaa taarifa za kila siku, kila wiki na kila mwezi za orodha za ukaguzi wa mashine (machine checklists);
  12. Kusaidia katika maandalizi na utekelezaji wa ratiba za matengenezo ya kinga (preventive maintenance schedules);
  13. Kushiriki katika programu za usalama kazini na kuzingatia miongozo ya afya na usalama mahali pa kazi;
  14. Kushirikiana na wanatimu wengine katika kutambua na kutatua hitilafu za mitambo pamoja na kutoa suluhisho stahiki;
  15. Kushirikiana na Mafundi Teknolojia (Technicians) na timu nyingine za matengenezo ili kuhakikisha utatuzi wa changamoto za kiufundi unafanyika kwa ufanisi;
  16. Kuhakikisha matumizi sahihi, utunzaji na uhifadhi wa zana na vifaa vya kazi za mitambo; na
  17. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Cheti cha Ufundi Stadi Daraja la Tatu (Level III) katika Fitter Mechanics au fani nyingine inayohusiana kutoka taasisi inayotambuliwa. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika majukumu ya uhandisi au matengenezo ya mitambo ndani ya viwanda vya uzalishaji au usindikaji. Uzoefu wa kufanya kazi katika mifumo ya boiler au uzalishaji wa nishati (Power Generation) utakuwa sifa ya ziada. Awe na uwezo wa kufanya kazi za ufungaji, matengenezo na ukarabati wa vifaa vya mitambo kwa kuzingatia viwango vya usalama na ubora vinavyotakiwa.