- Kuandaa michoro ya CAD ya 2D na 3D kwa ajili ya mashine, vifaa na mipangilio ya kiwanda;
- Kuandaa michoro ya fabrication na assembly yenye vipimo sahihi;
- Kushirikiana kwa karibu na wahandisi, wasanifu na timu za uzalishaji ili kubadilisha mawazo na dhana kuwa michoro inayoweza kutekelezeka;
- Kufanyia marekebisho na kusasisha michoro kulingana na maoni na mabadiliko ya usanifu;
- Kuhakikisha michoro inakidhi viwango vya sekta, kanuni za usalama na mahitaji ya kampuni;
- Kutunza nyaraka sahihi na mfumo wa udhibiti wa matoleo (version control) ya michoro yote;
- Kutoa msaada wa kiufundi kwa timu za uzalishaji;
- Kusaidia kutatua changamoto zinazohusiana na usanifu wakati wa uzalishaji;
- Kuandaa mipangilio ya miradi mipya na kupendekeza maboresho ya vifaa na mashine zilizopo;
- Kuratibu shughuli za ofisi ya michoro (Drawing Office);
- Kuwasaidia wahandisi wa kiwanda katika kutafsiri michoro;
- Kufanyia marekebisho michoro kulingana na mahitaji ya mteja; na
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na Stashahada (Diploma) au Shahada ya Kwanza (Bachelor Degree) katika Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Uhandisi wa Viwanda (Industrial Engineering) au fani nyingine ya kiufundi inayohusiana kutoka taasisi inayotambulika.
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sita (6) katika shughuli za usanifu kwa kutumia Kompyuta (Computer Aided Design - CAD) ndani ya sekta ya viwanda, uzalishaji mkubwa wa kilimo au fani nyingine inayolingana na hiyo.