Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Mchambuzi wa Maabara

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 3

Muhtasari wa nafasi

  1. Kukusanya na kuandaa sampuli kwa ajili ya uchambuzi wa maabara kutoka maeneo mbalimbali ya mchakato wa uzalishaji, mifumo ya maji na vituo vya kutibu majitaka;
  2. Kusaidia kufuatilia ubora wa maji ya bomba, maji ya mchakato wa uzalishaji na maji taka yanayotolewa ili kuhakikisha yanakidhi viwango vya kisheria na usalama;
  3. Kutunza kumbukumbu sahihi za vipimo vya maabara, matokeo ya uchambuzi na shughuli za kila siku za maabara;
  4. Kusafisha, kuendesha na kutunza vifaa na vyombo vya maabara kwa mujibu wa taratibu za kawaida za uendeshaji;
  5. Kusaidia shughuli za kuongeza kemikali katika michakato ya kutibu maji na usimamizi wa majitaka;
  6. Kuzingatia taratibu za usalama wa maabara na miongozo ya kushughulikia kemikali na utupaji wa taka;
  7. Kuwasilisha matokeo ya vipimo kwa Mkemia kwa ajili ya uchambuzi zaidi au hatua zinazohitajika za marekebisho;
  8. Kushiriki katika programu za ufuatiliaji wa mazingira ikiwemo ubora wa maji taka yanayotolewa na shughuli za kituo cha kutibu majitaka;
  9. Kusaidia programu za udhibiti wa ubora na mipango ya maboresho endelevu ndani ya maabara; na
  10. Kutekeleza majukumu mengine yoyote yanayohusiana na kazi atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Stashahada (Diploma) katika Sayansi na Teknolojia ya Maabara (Laboratory Science and Technology) au sifa nyingine inayolingana na hiyo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili (2) katika shughuli za maabara; uzoefu katika sekta ya sukari au viwanda vingine vya usindikaji utakuwa sifa ya ziada.