Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi Mashine Karakana

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kuendesha mashine za karakana kama vile lathe, milling, drilling na shaping machine kwa ajili ya kutengeneza vipuri na sehemu za mitambo kwa usahihi wa hali ya juu;
  2. Kuandaa mashine kwa ajili ya kazi, kuchagua vifaa sahihi vya kukatia (cutting tools) na kurekebisha mipangilio ya mashine kulingana na kazi inayotakiwa kufanyika;
  3. Kuripoti upotevu wa zana na vifaa vya kazi kwa msimamizi husika;
  4. Kufanya matengenezo ya kawaida ya mashine, usafishaji na ulainishaji (lubrication) ili kuhakikisha mashine zinafanya kazi kwa ufanisi;
  5. Kuandaa orodha ya vipuri vinavyohitajika kwa mashine mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za karakana zinaendelea bila usumbufu;
  6. Kuandaa na kuhifadhi zana zinazohitajika kwa shughuli za machining;
  7. Kusoma na kutafsiri michoro ya uhandisi (engineering drawings), blueprints na maelekezo ya kiufundi kwa ajili ya kutengeneza vipuri na sehemu za mitambo;
  8. Kutunza kumbukumbu sahihi za kazi zilizokamilika, vifaa vilivyotumika na utendaji wa mashine;
  9. Kudumisha usafi, mpangilio mzuri na mazingira salama katika eneo la karakana;
  10. Kufanya hesabu za msingi za machining zinazohitajika katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za karakana;
  11. Kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya mashine, zana na vifaa vya karakana;
  12. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na NTA Level III katika Welding and Fabrication au sifa nyingine inayolingana na hiyo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili (2) katika shughuli za karakana ya mashine (Machine Shop).

Awe na ujuzi wa kutumia mashine za karakana kama vile lathe, milling, drilling na shaping machine kwa ajili ya kutengeneza na kurekebisha vipuri vya mitambo.

Awe na uwezo wa kusoma na kutafsiri michoro ya kiufundi na kutumia vifaa vya kupimia kwa usahihi.

Awe na uelewa wa taratibu za usalama kazini, utunzaji wa mashine na matumizi sahihi ya zana za karakana