Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi wa Instrumentation

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kufunga, kupima na kufanya matengenezo ya vifaa vya kupimia na kudhibiti michakato (field instruments) ikiwemo pressure transmitters, flow meters, temperature sensors na level indicators katika maeneo ya uzalishaji na uzalishaji wa nishati;
  2. Kusaidia katika kufanya kalibresheni (calibration) na utatuzi wa hitilafu za mifumo ya udhibiti (control loops) na vifaa vya instrumentation ili kuhakikisha vipimo na taarifa za mrejesho (feedback) kwa ajili ya udhibiti wa michakato vinakuwa sahihi;
  3. Kusaidia katika ukaguzi na matengenezo ya Programmable Logic Controllers (PLCs), mifumo ya SCADA na nyaya za instrumentation ili kubaini hitilafu, uchakavu au changamoto za utendaji;
  4. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, matengenezo ya kinga (preventive maintenance) na kutunza kumbukumbu za vifaa vya instrumentation;
  5. Kusaidia katika ufungaji na uanzishaji (commissioning) wa vifaa vipya vya instrumentation na mifumo ya udhibiti;
  6. Kusaidia timu za matengenezo wakati wa kusimamisha uzalishaji kwa ajili ya matengenezo (plant shutdowns) na wakati wa kuanzisha upya shughuli za uzalishaji (start-ups);
  7. Kutunza kumbukumbu sahihi za kalibresheni, ukarabati na ubadilishaji wa vifaa vya instrumentation;
  8. Kuhakikisha shughuli zote za instrumentation zinafanyika kwa kuzingatia viwango vya usalama, ubora na taratibu za kazi zilizowekwa;
  9. Kushirikiana na timu za umeme na mitambo katika kutatua changamoto zinazohusisha mifumo mbalimbali ya vifaa vya uzalishaji;
  10. Kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia hitilafu au tahadhari (alarms) za instrumentation ili kupunguza usumbufu wa shughuli za uzalishaji;
  11. Kutoa taarifa kwa msimamizi kuhusu hitilafu, kasoro au hali zisizo za kawaida zinazobainika katika vifaa vya instrumentation;
  12. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Cheti cha Ufundi Stadi Daraja la Pili (Level II) au Daraja la Tatu (Level III) katika Instrumentation, Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering), Elektroniki (Electronics), au fani nyingine inayohusiana kutoka taasisi ya mafunzo ya ufundi au kiufundi inayotambuliwa. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka miwili (2) katika shughuli za vifaa vya kupimia na kudhibiti michakato ya viwandani (Industrial Instrumentation and Control Systems).

Awe na uelewa wa msingi wa mifumo ya instrumentation, kalibresheni ya vifaa, mifumo ya udhibiti wa michakato, PLCs, SCADA na vifaa vingine vinavyotumika katika mazingira ya viwandani. Uzoefu wa kufanya kazi katika viwanda vya usindikaji wa sukari na/au mitambo ya uzalishaji wa nishati (Power Generation Operations) utazingatiwa kuwa sifa ya ziada. Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vya usalama, ubora na taratibu za uendeshaji wa mifumo ya instrumentation na udhibiti wa michakato.