- Kupima, kukata, kupinda, kuunda na kuunganisha vifaa vya metali kulingana na mahitaji ya kazi husika;
- Kusoma na kutafsiri michoro ya kiufundi (technical drawings), blueprints na maelekezo ya fabrication ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa usahihi;
- Kuzingatia taratibu za afya, usalama na utunzaji wa mazingira mahali pa kazi wakati wote wa utekelezaji wa shughuli za fabrication;
- Kufanya kazi za kulehemu (welding) na fitting kwa ajili ya kuunganisha miundo ya vyuma na sehemu mbalimbali za mitambo;
- Kuendesha na kutumia vifaa na mashine za fabrication kama vile mashine za kukata vyuma, grinder, drill, press na vifaa vya kulehemu;
- Kukagua kazi zilizokamilika ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya ubora, usahihi na vipimo vilivyoainishwa;
- Kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya zana, vifaa na mashine zinazotumika katika shughuli za fabrication;
- Kudumisha usafi na mpangilio mzuri wa eneo la kazi na vifaa vya fabrication;
- Kuripoti changamoto, kasoro au hitilafu zozote zinazobainika wakati wa utekelezaji wa kazi kwa msimamizi husika;
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na NTA Level III katika Welding and Fabrication au sifa nyingine inayolingana na hiyo kutoka taasisi inayotambuliwa.
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika shughuli za kulehemu (Welding) na uundaji wa miundo ya vyuma (Fabrication).
Awe na uwezo wa kusoma na kutafsiri michoro ya kiufundi, blueprints na maelekezo ya fabrication.
Awe na ujuzi wa kutumia vifaa na mashine za fabrication kama vile mashine za kukata vyuma, grinder, drill, press na vifaa vya kulehemu.
Awe na uelewa wa viwango vya ubora, afya, usalama na utunzaji wa mazingira vinavyohusiana na shughuli za welding na fabrication.