- Kuendesha vacuum pans na vifaa vyake vinavyohusiana wakati wa uchemshaji wa sukari ili kuzalisha fuwele za sukari zenye ubora wa juu;
- Kufuatilia shinikizo la pan, halijoto, brix na purity ili kuhakikisha ukristalishaji sahihi wa sukari;
- Kudhibiti uingizaji wa massecuite, syrup na malighafi nyingine kwenye pan kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa;
- Kurekebisha vigezo vya uchemshaji ili kuhakikisha ukuaji bora wa fuwele za sukari (grain development) na urejeshaji wa sukari (sugar recovery);
- Kufuatilia vacuum pumps, condensers na vifaa vingine saidizi ili kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo;
- Kuchukua sampuli za uchemshaji wa sukari na kufanya vipimo vya msingi vya eneo la kazi ili kufuatilia maendeleo ya ukristalishaji;
- Kushirikiana na maabara na timu za mchakato wa uzalishaji katika kuhakikisha ubora wa bidhaa na kufanya marekebisho ya mchakato pale inapohitajika;
- Kutunza kumbukumbu sahihi za mizunguko ya uchemshaji, batch za pan na viashiria vya utendaji wa vifaa;
- Kusafisha na kutunza vacuum pans, seed magma mixers pamoja na zana na vifaa vinavyohusika;
- Kuzingatia taratibu za usalama wakati wa shughuli za uchemshaji na kuripoti hali yoyote isiyo salama;
- Kuwasiliana na control room na watumishi wa maeneo ya uzalishaji ili kuhakikisha shughuli zinafanyika kwa uratibu mzuri;
- Kusaidia katika kutatua changamoto zinazohusiana na pan na kuripoti matatizo magumu kwa wasimamizi husika;
- Kushiriki katika shughuli za matengenezo ya kawaida na matengenezo ya kinga ya vifaa vya pan boiling; na
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na angalau Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika shughuli za uchemshaji wa sukari (sugar boiling), ukristalishaji wa sukari (crystallization operations) au fani nyingine inayohusiana.
Awe na Cheti cha National Sugar Institute (NSI); sifa hii itakuwa nyongeza.