- Kufunga, kuunganisha, kupanga kwa usahihi (align) na kufanya fitting ya vifaa vya mitambo, mashine na sehemu zake;
- Kuandaa vipuri kwa ajili ya shughuli zilizopangwa;
- Kubadilisha sehemu za mashine zilizochakaa au zenye hitilafu kwa kutumia zana na mbinu sahihi;
- Kutunza kumbukumbu za matengenezo, taarifa za huduma na matumizi ya vipuri;
- Kuhakikisha uzingatiaji wa taratibu za afya, usalama na utunzaji wa mazingira mahali pa kazi; na
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na Cheti cha NTA Level III katika Fitter Mechanics. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika shughuli za karakana ya mashine (Machine Shop).