Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Mwendeshaji wa Mfumo wa DCS – Kitengo cha Evaporator

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kuendesha na kufuatilia michakato ya uzalishaji kupitia mfumo wa Distributed Control System (DCS) au SCADA kutoka chumba cha udhibiti (Control Room);
  2. Kuhakikisha uendeshaji bora wa vifaa vya kiwanda na michakato ya uzalishaji kwa kurekebisha vigezo na mifumo ya udhibiti wa mchakato;
  3. Kufuatilia boilers, mifumo ya uzalishaji wa umeme, shughuli za milling, clarification, evaporation, crystallization, mitambo ya kutibu maji na vitengo vingine vya mchakato wa uzalishaji;
  4. Kuhakikisha kuanzishwa, uendeshaji na kusimamishwa kwa vifaa vya kiwanda kunafanyika kwa mujibu wa taratibu za kawaida za uendeshaji;
  5. Kufuatilia viashiria vya uzalishaji, alama za tahadhari (alarms) na hali za dharura, na kuchukua hatua za marekebisho pale inapohitajika;
  6. Kuwasiliana na waendeshaji wa maeneo ya kazi (field operators) na mafundi wa michakato ya uzalishaji ili kuratibu shughuli za uendeshaji na marekebisho ya mchakato;
  7. Kutunza kumbukumbu za uzalishaji, matukio ya kusimama kwa shughuli (downtime), mkengeuko wa michakato na kuandaa taarifa kwa ajili ya mapitio ya menejimenti;
  8. Kufanya ukaguzi wa kawaida wa mifumo ya mchakato wa uzalishaji na kumjulisha Mhandisi wa Mchakato (Process Engineer) kuhusu hali zisizo za kawaida au mahitaji ya matengenezo;
  9. Kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vya mazingira kwa kufuatilia na kudhibiti majitaka na hewa chafu zinazozalishwa;
  10. Kusaidia utekelezaji wa taratibu za afya, usalama na mazingira ndani ya chumba cha udhibiti na maeneo ya uzalishaji;
  11. Kushiriki katika taratibu za makabidhiano ya zamu na kuhakikisha mawasiliano sahihi kati ya zamu mbalimbali;
  12. Kusimamia na kutoa mwongozo kwa Waendeshaji wa Chumba cha Udhibiti (Control Room Operators) na watumishi wengine walio chini yake wakati wa zamu; na
  13. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake

Mahitaji

Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika shughuli za uendeshaji wa mitambo ya usindikaji (processing plant operations), ikiwezekana katika sekta ya sukari.

Awe na Cheti cha National Sugar Institute (NSI); sifa hii itakuwa nyongeza.