Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Mwendeshaji Mwandamizi wa Pani za Uchemshaji wa Sukari

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 2

Muhtasari wa nafasi

  1. Kusimamia na kuwaelekeza Mafundi wa Uchemshaji wa Sukari (Pan Boiling Technicians) katika kutekeleza taratibu na mbinu sahihi za uchemshaji;
  2. Kuendesha na kufuatilia vacuum pans ili kuhakikisha ukristalishaji (crystallization) unafanyika kwa ufanisi wakati wa mchakato wa uchemshaji wa sukari;
  3. Kuhakikisha shughuli za seeding, graining na vigezo vya uchemshaji wa massecuite vinafuatwa na kudumishwa kwa usahihi wakati wote;
  4. Kuchambua na kudhibiti kiwango cha syrup kinachoingia, halijoto, kiwango cha vacuum na mwenendo wa uchemshaji (boiling curves) kwa kila batch;
  5. Kufuatilia brix, purity na ukuaji wa fuwele za sukari (crystal growth) ili kuhakikisha ubora unaotakiwa wa sukari unapatikana;
  6. Kuratibu mizunguko ya uchemshaji wa A, B na C strikes kulingana na mahitaji ya uzalishaji na malengo ya urejeshaji wa sukari (recovery goals);
  7. Kuhakikisha uendeshaji bora wa vacuum pumps, condensers na mifumo ya kupasha joto inayotumika katika pan house;
  8. Kushirikiana na maabara na wafanyakazi wa control room ili kudumisha ubora wa bidhaa na kufanya marekebisho ya vigezo vya mchakato pale inapohitajika;
  9. Kutunza kumbukumbu sahihi za mizunguko ya uchemshaji, ubora wa massecuite na utendaji wa vacuum pans;
  10. Kutoa mafunzo na mwongozo kwa watumishi wa ngazi za chini wanaohusika na uchemshaji wa sukari ili kuhakikisha taratibu zinafuatwa ipasavyo;
  11. Kubaini na kuripoti kwa Pan Boiling Supervisor mkengeuko wowote wa mchakato au hitilafu za vifaa vinavyoweza kuathiri uzalishaji;
  12. Kushiriki katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za uzalishaji za kila siku ili kuoanisha shughuli za pan boiling na shughuli za milling pamoja na centrifuge;
  13. Kuhakikisha usafi na mazingira bora ya kazi katika maeneo ya pan boiling na vifaa vyake saidizi;
  14. Kuzingatia miongozo ya usalama na utunzaji wa mazingira wakati wa shughuli za pan house;
  15. Kushiriki katika shughuli za kusimamisha uzalishaji kwa ajili ya matengenezo (shutdown) na matengenezo ya vifaa vya pan house; na
  16. Kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) au sifa ya juu zaidi.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sita (6) katika shughuli za uchemshaji wa sukari (Sugar Pan Boiling Operations).

Awe na Cheti cha National Sugar Institute (NSI); sifa hii itakuwa nyongeza.