Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi Teknolojia wa Matengenezo ya Kinga.

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kuandaa na kutekeleza ratiba za matengenezo ya vifaa na miundombinu;
  2. Kuweka vipaumbele vya kazi kulingana na uharaka wake, mzigo wa kazi na rasilimali zilizopo;
  3. Kushirikiana kwa karibu na mafundi wa matengenezo, wahandisi na timu za uendeshaji;
  4. Kuwasiliana na wasambazaji wa vifaa na vipuri kwa ajili ya upatikanaji wa vipuri na zana;
  5. Kukadiria muda, nguvu kazi na gharama za kazi za matengenezo;
  6. Kufuatilia na kusimamia akiba ya vipuri ili kuepusha ucheleweshaji wa shughuli za matengenezo;
  7. Kutumia CMMS (Computerized Maintenance Management Systems) kama ERP au Maximo kurekodi na kufuatilia maagizo ya kazi (work orders);
  8. Kuandaa taarifa za shughuli za matengenezo, gharama na viashiria vya utendaji;
  9. Kukagua miundombinu na vifaa ili kubaini hatari zinazoweza kujitokeza na kuhakikisha taratibu za usalama zinafuatwa;
  10. Kuhakikisha uzingatiaji wa viwango na kanuni za sekta husika; na
  11. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Stashahada (Diploma) katika Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Uhandisi wa Viwanda (Industrial Engineering) au fani nyingine ya kiufundi inayohusiana kutoka taasisi inayotambulika.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sita (6) katika upangaji wa matengenezo (maintenance planning) ndani ya sekta ya viwanda, uzalishaji mkubwa wa kilimo au fani nyingine inayolingana na hiyo.

Awe na uzoefu wa kutumia mifumo na programu za usimamizi wa matengenezo kama vile SAP Plant Maintenance, CMMS na Microsoft Office.