Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi Mwandamizi wa Instrumentation

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 3

Muhtasari wa nafasi

  1. Kufunga, kupima na kufanya matengenezo ya vifaa vya kupimia na kudhibiti michakato (field instruments) ikiwemo pressure transmitters, flow meters, temperature sensors na level indicators katika maeneo ya uzalishaji na uzalishaji wa nishati;
  2. Kufanya kalibresheni (calibration) na utatuzi wa hitilafu katika mifumo ya udhibiti (control loops) na vifaa vya instrumentation ili kuhakikisha vipimo na taarifa za mrejesho (feedback) kwa ajili ya udhibiti wa michakato vinakuwa sahihi;
  3. Kukagua na kufanya matengenezo ya Programmable Logic Controllers (PLCs), mifumo ya SCADA na nyaya za instrumentation ili kubaini hitilafu, uchakavu au changamoto za utendaji;
  4. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, matengenezo ya kinga (preventive maintenance) na kutunza kumbukumbu za vifaa vya instrumentation;
  5. Kusaidia katika ufungaji na uanzishaji (commissioning) wa vifaa vipya vya instrumentation na mifumo ya udhibiti;
  6. Kusaidia timu za matengenezo wakati wa kusimamisha uzalishaji kwa ajili ya matengenezo (plant shutdowns) na wakati wa kuanzisha upya shughuli za uzalishaji (start-ups);
  7. Kutunza kumbukumbu sahihi za kalibresheni, ukarabati na ubadilishaji wa vifaa vya instrumentation;
  8. Kuhakikisha shughuli zote za instrumentation zinafanyika kwa kuzingatia viwango vya usalama, ubora na taratibu za kazi zilizowekwa;
  9. Kushirikiana na timu za umeme na mitambo katika kutatua changamoto zinazohusisha mifumo mbalimbali ya vifaa vya uzalishaji;
  10. Kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia hitilafu au tahadhari (alarms) za instrumentation ili kupunguza usumbufu wa shughuli za uzalishaji;
  11. Kutoa mwongozo wa kiufundi kwa mafundi wa ngazi za chini katika masuala ya instrumentation na mifumo ya udhibiti;
  12. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake

Mahitaji

Awe na Cheti cha Ufundi Stadi Daraja la Tatu (Level III Certificate) katika Instrumentation, Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering), Elektroniki (Electronics), au fani nyingine inayohusiana kutoka taasisi ya mafunzo ya ufundi au kiufundi inayotambuliwa. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sita (6) katika shughuli za vifaa vya kupimia na kudhibiti michakato ya viwandani (Industrial Instrumentation and Control Systems).

Awe na uelewa wa mifumo ya udhibiti wa michakato, kalibresheni ya vifaa vya instrumentation, PLCs, SCADA na vifaa vingine vinavyotumika katika mazingira ya viwandani. Uzoefu wa kufanya kazi katika viwanda vya usindikaji wa sukari na/au mitambo ya uzalishaji wa nishati (Power Generation Operations) utazingatiwa kuwa sifa ya ziada. Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vya usalama, ubora na taratibu za uendeshaji wa mifumo ya instrumentation na udhibiti wa michakato.