- Kupanga, kuratibu na kudhibiti shughuli za matengenezo ya mitambo katika kiwanda cha sukari ili kuhakikisha ufanisi wa shughuli za uzalishaji;
- Kuongoza shughuli za matengenezo na ukarabati wa boiler, vifaa vya kitengo cha kusaga miwa, pampu, conveyor na mashine nyingine za kiwanda;
- Kuratibu na kusimamia shughuli za kila siku za karakana ya kiwanda ili kuhakikisha kazi za fabrication, welding, machining na ukarabati zinafanyika kwa ufanisi;
- Kuandaa na kutekeleza programu za matengenezo ya kinga (preventive), matengenezo ya utabiri (predictive) na matengenezo ya kurekebisha hitilafu (corrective) kwa vifaa vyote vya mitambo;
- Kufuatilia utendaji wa mifumo ya mitambo na kupendekeza maboresho au mabadiliko ya vifaa ili kuongeza ufanisi na kutegemewa kwake;
- Kusimamia matengenezo na uendeshaji salama wa mifumo ya uzalishaji na usambazaji wa mvuke ndani ya kiwanda;
- Kusimamia masuala ya mitambo katika mchakato wa kusaga miwa ili kuhakikisha crushers, mills, gearboxes na drives zinafanya kazi kwa kiwango bora;
- Kusimamia upangiliaji sahihi (alignment), usawazishaji (balancing) na kalibresheni ya vifaa vinavyozunguka;
- Kuhakikisha shughuli zote za mitambo zinafanyika kwa kuzingatia viwango vya usalama vya kiwanda, sheria na kanuni za mamlaka husika pamoja na mahitaji ya mazingira;
- Kuratibu shughuli za ukarabati wa dharura ili kupunguza muda wa kusimama kwa uzalishaji na kurejesha shughuli za kiwanda kwa haraka;
- Kuandaa bajeti za matengenezo ya mitambo na kudhibiti matumizi ya gharama ndani ya viwango vilivyoidhinishwa;
- Kusimamia akiba ya vipuri, vifaa na zana muhimu za karakana ili kuhakikisha upatikanaji wake wakati wote;
- Kuandaa taratibu za kawaida za uendeshaji (SOPs) kwa shughuli za matengenezo ya mitambo na kuhakikisha zinafuatwa na timu za kiufundi;
- Kufanya tathmini za mara kwa mara za hatari zinazohusiana na mifumo ya mitambo na kutekeleza hatua stahiki za kudhibiti hatari hizo;
- Kusimamia ukaguzi na upimaji wa vyombo vya shinikizo (pressure vessels), vifaa vya kunyanyulia mizigo na mifumo ya usalama wa mitambo;
- Kushiriki katika miradi ya upanuzi wa kiwanda ikiwemo ufungaji na uanzishaji wa mashine na vifaa vipya;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa menejimenti kuhusu masuala ya uhandisi wa mitambo;
- Kutoa mafunzo, mwongozo na kukuza uwezo wa watumishi wa karakana na timu za matengenezo;
- Kutekeleza programu za kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati na kupendekeza suluhisho za mitambo zinazookoa nishati;
- Kuwasiliana na wakandarasi na watoa huduma wa nje kwa ajili ya kazi maalumu za mitambo;
- Kuhakikisha kumbukumbu na taarifa zote za shughuli za matengenezo ya mitambo na historia ya vifaa zinatunzwa ipasavyo;
- Kuratibu na kusimamia shughuli za ukarabati mkubwa wa vifaa (overhauls) na programu za matengenezo wakati wa kusimamisha uzalishaji kila mwaka;
- Kushiriki katika mikutano ya kiwanda inayojumuisha idara mbalimbali ili kuhakikisha shughuli za mitambo zinaendana na malengo ya uzalishaji;
- Kuongoza mipango ya maboresho endelevu katika mbinu na shughuli za matengenezo ya mitambo;
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake; na
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na Shahada ya Kwanza katika Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Uhandisi wa Electromechanical (Electromechanical Engineering) au Uhandisi wa Viwanda (Industrial Engineering) kutoka taasisi inayotambulika.
Awe amesajiliwa na bodi au taasisi husika za kitaaluma za uhandisi; sifa hii itakuwa nyongeza.
Awe na cheti katika Usimamizi wa Matengenezo (Maintenance Management) au mafunzo mengine ya kiufundi yanayohusiana; sifa hii itakuwa nyongeza.
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika matengenezo ya mitambo na usimamizi wa karakana ndani ya viwanda vya uzalishaji au uzalishaji wa sukari.
Uzoefu katika matengenezo ya boiler, mills, pampu na mifumo mingine ya mitambo utakuwa sifa ya ziada.