Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi wa Umeme

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, matengenezo na ukarabati wa vifaa na mifumo ya umeme katika kiwanda na maeneo ya shughuli za kilimo;
  2. Kusaidia katika uendeshaji na ufuatiliaji wa mifumo ya uzalishaji wa umeme;
  3. Kutambua na kurekebisha hitilafu za umeme pamoja na kushughulikia matatizo ya vifaa ili kupunguza muda wa kusimama kwa shughuli za uzalishaji;
  4. Kutekeleza kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme chini ya usimamizi wa watumishi wa ngazi za juu;
  5. Kuhakikisha nyaya, kebo na miunganisho ya mifumo ya umeme inafungwa na kuunganishwa kwa mujibu wa viwango vya kiufundi vinavyotakiwa;
  6. Kudumisha usafi, usalama na mpangilio mzuri katika maeneo ya kazi za umeme;
  7. Kutunza na kulinda zana, vifaa na malighafi zinazotumika katika kazi za umeme;
  8. Kuzingatia taratibu na viwango vya usalama wa umeme wakati wa shughuli za matengenezo na uendeshaji wa mifumo ya umeme;
  9. Kuandaa taarifa za msingi za matengenezo na kutunza kumbukumbu za kazi zilizotekelezwa;
  10. Kusaidia katika upimaji na uanzishaji (testing and commissioning) wa vifaa vipya vya umeme vilivyofungwa;
  11. Kuripoti kwa Fundi Teknolojia Mwandamizi wa Umeme hitilafu, kasoro au hatari zozote zinazoweza kuathiri usalama au utendaji wa vifaa ili hatua za haraka zichukuliwe;
  12. Kushiriki katika shughuli za zamu za kufuatilia upatikanaji wa umeme na uendeshaji wa vifaa vya umeme;
  13. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Stashahada (Diploma) katika Uhandisi wa Umeme (Electrical Engineering) au Electrical Installation kutoka taasisi inayotambuliwa. Awe amesajiliwa na Bodi ya Wahandisi Tanzania (Engineers Registration Board - ERB) au awe na cheti kingine cha kitaaluma kinacholingana na hicho; sifa hii itakuwa nyongeza.

Awe na uelewa wa mifumo ya umeme ya viwandani, ufungaji wa vifaa vya umeme, matengenezo na utatuzi wa hitilafu za umeme. Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vya usalama wa umeme, kanuni za kitaaluma na taratibu za kazi zilizowekwa. Uzoefu wa kufanya kazi katika viwanda vya uzalishaji, usindikaji au uzalishaji wa nishati utazingatiwa kuwa sifa ya ziada.