Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Mwendeshaji Mwandamizi wa Mashine za Centrifuge za Sukari Ghafi

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 3

Muhtasari wa nafasi

  1. Kuendesha mashine na vifaa vinavyotumika katika mchakato wa uzalishaji ikiwemo uchimbaji wa juisi ya miwa (juice extraction), usafishaji wa juisi (clarification), uvukizaji (evaporation), ukristalishaji (crystallization) na ukaushaji (drying);
  2. Kufuatilia vigezo vya mchakato wa uzalishaji na kuripoti mkengeuko au hali zisizo za kawaida kwa Fundi Teknolojia Mwandamizi wa Uzalishaji (Senior Processing Technician);
  3. Kusaidia kurekebisha mifumo ya udhibiti wa mchakato ili kudumisha ubora wa bidhaa na kuongeza ufanisi wa uzalishaji;
  4. Kutunza kumbukumbu za taarifa za uendeshaji kama vile halijoto, shinikizo, viwango vya mtiririko na kiasi cha uzalishaji;
  5. Kufanya ukaguzi wa kawaida wa vifaa na kuhakikisha usafi pamoja na mpangilio mzuri wa eneo la kazi;
  6. Kushiriki katika matengenezo madogo ya vifaa na kuripoti hitilafu zozote kwa timu ya matengenezo;
  7. Kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vya afya, usalama na mazingira (HSE) katika shughuli zote za uendeshaji;
  8. Kushiriki katika ukaguzi wa ubora wa bidhaa kwa kushirikiana na timu ya Uhakiki wa Ubora (Quality Assurance);
  9. Kusaidia kutatua changamoto za uendeshaji na kutekeleza hatua za marekebisho;
  10. Kutoa msaada katika mafunzo ya waendeshaji na mafundi wapya kwa mujibu wa maelekezo yatakayotolewa;
  11. Kuhakikisha mawasiliano na makabidhiano sahihi ya shughuli za uendeshaji kati ya zamu moja na nyingine; na
  12. Kutekeleza majukumu mengine yoyote atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano (5) katika shughuli za uendeshaji wa Mashine za Batch Centrifugal.

Awe na Cheti cha National Sugar Institute (NSI); sifa hii itakuwa nyongeza.