Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Afisa wa Maboresho Endelevu.

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 3

Muhtasari wa nafasi

  1. Kuongoza na kusaidia utekelezaji wa mipango ya maboresho endelevu katika mistari yote ya uzalishaji;
  2. Kubaini uzembe, upotevu wa rasilimali na fursa za kupunguza gharama za uendeshaji;
  3. Kukusanya na kuchambua takwimu za uzalishaji ili kubaini mwenendo wa utendaji;
  4. Kuandaa mapendekezo yanayotegemea ushahidi kwa ajili ya maboresho ya shughuli za uendeshaji;
  5. Kufuatilia viashiria muhimu vya utendaji (KPIs) ili kuhakikisha maboresho yaliyofanyika yanaendelea kudumishwa;
  6. Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kuhusu zana za Lean kama vile 5S, Value Stream Mapping, SMED na Kanban;
  7. Kutoa mwongozo kuhusu matumizi ya mbinu za Six Sigma;
  8. Kuandaa maelekezo ya kazi yaliyo wazi na kuhakikisha mabadiliko yanatekelezwa ipasavyo;
  9. Kushirikiana kwa karibu na timu za uzalishaji, uhandisi na matengenezo;
  10. Kuwasiliana na kushirikiana na idara za kiufundi ili kuhakikisha uzingatiaji wa mahitaji ya usalama na ergonomics;
  11. Kujenga mahusiano mazuri ili kupata ushiriki na uungwaji mkono wa wafanyakazi katika mabadiliko yanayotekelezwa;
  12. Kufanya kazi za uandishi wa mabango, uchoraji, uwekaji wa lebo kwenye vifaa na alama mbalimbali za maelekezo;
  13. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa

Mahitaji

Awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV Certificate) au NTA Level I pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu (3) katika shughuli za maboresho endelevu (Continuous Improvement) ndani ya sekta ya viwanda, uzalishaji mkubwa wa kilimo au fani nyingine inayolingana na hiyo.