Rudi kwenye nafasi zote

Ajira

Fundi Mitambo wa Kitengo cha Kusaga Miwa.

Muda Wote Idara: Uendeshaji wa Kiwanda Mahali: Mbigiri - Kilosa Tarehe ya Mwisho: Juni 8, 2026 Idadi ya nafasi: 1

Muhtasari wa nafasi

  1. Kufanya matengenezo ya kawaida na ukarabati wa vifaa vya mitambo kama vile mashine za kusaga miwa (mills), conveyor, gearbox na mitambo mingine ya kiwanda;
  2. Kusaidia kutambua na kutatua hitilafu za mitambo pamoja na kufanya matengenezo ya kurekebisha kasoro zilizobainika;
  3. Kufanya kazi za kufunga na kuunganisha vifaa vya mitambo (fitting), kulehemu, kukata, kusaga na kutengeneza vifaa mbalimbali kulingana na mahitaji ya matengenezo na ukarabati;
  4. Kufanya ukaguzi wa mashine, usafishaji, ulainishaji (lubrication) na marekebisho ya sehemu za mitambo ili kuhakikisha zinafanya kazi kwa ufanisi;
  5. Kushiriki katika ufungaji na uanzishaji wa vifaa vipya vya mitambo;
  6. Kusaidia kutunza kumbukumbu sahihi za shughuli za matengenezo na kazi zilizokamilishwa;
  7. Kuzingatia taratibu za usalama na kuhakikisha kazi zote za matengenezo zinafanyika kwa kuzingatia mazingira salama ya kazi;
  8. Kuripoti kwa msimamizi kasoro zozote za mitambo au dalili za hitilafu zinazoweza kusababisha uharibifu wa vifaa ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati;
  9. Kushiriki katika shughuli za matengenezo ya kusimamisha uzalishaji kwa mpango maalum (planned shutdown maintenance) pamoja na ukarabati mkubwa wa vifaa (overhauls);
  10. Kuhakikisha matumizi sahihi na utunzaji wa zana, vifaa na miundombinu ya karakana;
  11. Kudumisha usafi na mpangilio mzuri wa maeneo ya kazi; na
  12. Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.

Mahitaji

Awe na Stashahada (Diploma) katika Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Matengenezo ya Mitambo ya Viwandani (Industrial Maintenance), au fani nyingine inayohusiana na taaluma hiyo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitano (5) katika shughuli za matengenezo ya mitambo ya viwandani, ikiwezekana akiwa amefanya kazi katika viwanda vya sukari au mazingira yanayofanana na hayo.