- Kuhakikisha mashine na vifaa vinawekwa katika mkao sahihi (alignment), vinasawazishwa (levelling) na kufungwa imara katika maeneo yake ya kazi;
- Kuchagua pulleys, booms, braces, nyaya za kunyanyulia (cables) na vifaa vingine vinavyofaa kulingana na aina ya kazi inayotekelezwa;
- Kutathmini hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa kunyanyua na kusogeza vifaa vizito, hususan katika maeneo yenye nafasi ndogo au yaliyofungwa;
- Kusafisha, kuvivunja kwa utaratibu na kuhifadhi vifaa vya rigging baada ya kazi kukamilika;
- Kuhakikisha taratibu zote za usalama zinazingatiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na sera za kampuni;
- Kuandaa na kukagua njia zitakazotumika kusafirisha mizigo mizito ili kuhakikisha usalama wa usafirishaji;
- Kuzingatia viwango vya uzito vinavyoruhusiwa na kukadiria kwa usahihi uzito salama wa vifaa, mashine, vipuri au malighafi vinavyopaswa kunyanyuliwa;
- Kuwasiliana na kuripoti changamoto au matatizo yoyote yanayojitokeza kwa msimamizi kwa hatua stahiki;
- Kushirikiana na timu za matengenezo, ufungaji na ukarabati katika shughuli za kunyanyua na kusogeza vifaa vizito;
- Kutekeleza majukumu mengine yoyote halali atakayopangiwa na msimamizi wake.
Muhtasari wa nafasi
Mahitaji
Awe na Cheti (Certificate) katika Uhandisi wa Mitambo (Mechanical Engineering), Fitting and Machining, au fani nyingine inayohusiana kutoka taasisi inayotambuliwa. Awe na vyeti vya kitaaluma vya ziada kama vile Certified Engineering Technician (CET) au Lean Six Sigma Green Belt, ambavyo vitakuwa sifa ya ziada. Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka sita (6) katika shughuli za rigging, ufundi wa fitting au matengenezo ya mitambo katika mazingira ya viwanda vya uzalishaji au usindikaji. Uzoefu wa kufanya kazi katika sekta ya sukari utazingatiwa kuwa sifa ya ziada.